GET /api/v0.1/hansard/entries/1319723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1319723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1319723/?format=api",
    "text_counter": 339,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja kuhusu Hotuba ya Rais. Ninampongeza Mhe. Rais kwa Hotuba yake ambayo imeangazia mambo mengi ambayo ameyatenda pamoja na utawala wake. Nikiangalia suala la walimu, kitu ambacho hakikuenda sawa ni ugawanyaji wa hawa walimu 56,000. Wangegawanywa sawa kwa yale maeneo Bunge 290. Eneo Bunge moja lingeweza kupata walimu 180 na kuzidi. Kwa baadhi yetu ambao tuna uhaba zaidi, tungeweza kukimu sehemu hiyo ya elimu. Tukizingatia usawa wa nafasi za kazi, ni muhimu siku za usoni nafasi zote iwapo ni kwa Idhara za Usalama na Huduma za Taifa zigawanywe kwa maeneo bunge na hapo tutasaidika zaidi. Ninampongeza Rais kwa uamuzi kwamba wale vijana ambao wanaenda kwa Huduma ya Taifa, wanapohitimu masomo, wapewe nafasi za kwanza kuajiriwa katika vikosi vya usalama humu nchini. Hilo ni jambo la kusaidia kwa maana ukiwaangalia hawa vijana, hawapati chochote lakini wanajitolea katika nyanja zote kuona kwamba wanahudumia taifa hili bila kuogopa, wasiwasi na hata bila kujali maslahi yao. Hatua hiyo ya Rais inastahili kupongezwa. Mradi huu wa nyumba zenye gharama nafuu unastahili kupongezwa tukizingatia kwamba tuko na wakati mgumu kabisa kiuchumi lakini Rais anajizatiti kuona miradi hii inaendelea. Ametupa matumaini watu wa Magarini kwamba hivi karibuni mradi huu utatufikia. Ni tamaa yetu kwamba mradi huu unapofika, tutabuni nafasi za kazi, na kupata makao kwa wale ambao hawawezi kupata nyumba za bei nafuu na kuishi katika mazingira mazuri. Kwa hakika Mheshimiwa Rais yuko na maono mazuri kwa nchi hii. Tatizo ni kwamba baadhi yetu sisi wananchi wa Kenya hatuna maono aliyonayo wala hatuwezi kuyaangazia kwa undani tukajua amelenga wapi. Tusikose kufahamu kwamba panapo mawimbi mazito ndipo palipo na mla. Mla ni mla leo, mla jana kalani? Hilo ndilo linatusumbua sisi. Tunataka kila kitu kifanyike sawasawa bila wasiwasi wowote kwa wakati ambao hata hauwezekani. Lazima tuwe na wakati mzuri wa kupea nchi kupona. Kufikia hivi sasa, nchi imeanza kupona polepole. Kwa Kiingereza tunasema: ‘ The country is now healing and we need to give it time.’"
}