GET /api/v0.1/hansard/entries/1319736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1319736,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1319736/?format=api",
    "text_counter": 352,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi. Nilifurahia sana Hotuba ya Rais. Rais hakutupea dawa ya kutuliza maumivu, yaani ruuku; bali alipeana dawa ya kutibu ugonjwa. Dawa ya ruuku, au ukipenda painkiller, inatumika kutuliza maumivu kidogo, ugonjwa ungalipo. Rais anajua kwamba Kenya inaugua wapi na hataki kutupatia dawa ya kutuliza maumivu bali anataka kututibu. Saa hii ni wakati wake wa kutibu ugonjwa. Kiongozi lazima atibu ugonjwa na sio kuubembeleza. Rais ameweka mikakati mizuri ya kutibu ugonjwa huu. Nilifurahia zaidi Rais alipotaja jamii zilizotengwa. Alisema mengi lakini la muhimu sana ni swala la mifugo. Tunaona kuwa Rais anazingatia masilahi yetu kwa sababu wakati mwingine, sehemu zingine zinapotajwa, wengine wanaumwa sana. Hii inaonyesha kuwa kuna kasoro kati yetu; hatuchukuliani kama Wakenya sote. Lakini Rais alitoa msimamo kuwa Wakenya wote ni Wakenya. Maswala ya mifugo ikitiliwa maanani basi uchumi utaimarika katika maeneo yaliyotengwa. Rais pia ameanza kutenda anayosema. Wiki iliyopita, tulimwona akitembelea jamii zilizotengwa na pia anatimiza ahadi zake. Kwa mfano, ameanzisha ujenzi wa barabara Lamu ambapo hatujakuwa na hata inchi moja ya lami kwa miaka sitini. Lakini Rais ameanzisha mradi huu na kweli tunaona kuwa atafanya yote anayosema. Rais pia alirejelea maswala ya uchumi samawati. Alisema kuwa ataweka tuvuti za kutua katika kila kaunti katika Mkoa wa Pwani kutoka Shimoni hadi Kiunga. Tumeona tovuti hizi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}