GET /api/v0.1/hansard/entries/1319737/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1319737,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1319737/?format=api",
    "text_counter": 353,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "zikijengwa na zikifunguliwa. Tovuti ya kutua ya Kiunga ndio tu iliyosalia na Rais alihaidi kuitengeneza. Tunatajaria kuwa itatengenezwa. Tovuti ya kutua ya Mkowe pia imepangiwa kutengenezwa. Hili likifanyika, tutaweza kuvua na kuhifadhi samaki wengi. Rais alizungumzia maswala ya uchumi samawati kutoka moyoni. Kwa hiyo, tunaimani kuwa biashara ya uvuvi itaendelezwa na itasaidia Wakenya wote. Wengine wakipanda majani chai, sisi tunavua samaki na hivi ndivyo tutaendeleza nchi yetu ya Kenya. Lakini watu wakitaka tu maendeleo katika maeneo yao wakati sehemu zingine zinaachwa nyuma, mwishowe sote tunaumia. Jambo ambalo sikulifurahia ni aliposema kuwa maafisa wa polisi watachukuliwa kutoka miongoni mwa makurutu wa NYS. Huu ni mpangilio mzuri lakini sehemu zingine kama kwetu vijana hawaendi sana NYS. Tunahofia kuwa tutakosa nafasi za Kenya Defence Forces (KDF) na polisi. Tunaomba Rais ahimize kuwa vijana asilimia 50 wachukuliwe kutoka NYS na asilimia 50 kutoka maeneo mengine. Vijana kutoka Lamu wamezoea kuchunga mifugo na kuvua samaki na wakienda NYS wanaona wanapoteza. Kusema kweli, tumeona walimu wakiajiriwa. Namba ya walimu ikiongezeka tutasaidika. Huko kwetu Lamu, waalimu wakifunza miaka mitatu tu wanakimbia kisha wakirudi wanapelekwa sehemu zingine na wanalipwa mishahara kama kawaida. Jambo hili linatutatiza sana kule kwetu. Rais anafutilia maswala ya elimu kwa karibu sana. Kwa mfano, anataka kujua kwa nini katika eneo Bunge la Lamu Mashariki ni mwanafunzi mmoja tu ndiye anafuzu kuenda chuo kikuu. Rais ameweka mikakati kamili na pia kutuhusisha viongozi wa sehemu hizi kuhusu jambo hili. Ukweli ni kwamba, Rais anatenda anayvosema. Tumpeni tu muda na tumuunge mkono ili atende kazi na uchumi wetu uimarike. Asante Bw. Spika wa Muda."
}