GET /api/v0.1/hansard/entries/1323777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1323777,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323777/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii nichangie mjadala huu ambao ni muhimu. Mtu yeyote ambaye hathamini mila yake ama hajui alikotoka, basi huenda hajui anaelekea wapi. Hii ni hali hatari ukiangalia vile Wakenya walivyo. Hoja hii inaangazia swala la vitu vyetu vyenye thamani ambavyo vimepelekwa nje ili kuhakisha kwamba havipelekwi tena nje. Pia, Hoja hii ikipitishwa, vile vitu ambavyo viko nje vitaregeshwa nchini. Mbunge mwenzangu alizungumzia swala la vigango vingi vilivyochukuliwa na kupelekwa ughaibuni. Vigango ni vitu ambavyo Wamijikenda walikuwa wakivienzi sana. Vilikuwa vinatumika kuleta amani, upendo na utaratibu wa mila za Wamijikenda. Mtu akifiwa na mtu wake, ni lazima kaburi hatimaye itoweke. Kigango, ambacho kilikuwa kikitengenezwa kutokana na mti madhubuti usiooza, kilikuwa kinawekwa na familia ya mwendazake wakijua The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}