GET /api/v0.1/hansard/entries/1323780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1323780,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323780/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Emurua Dikir, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Johana Kipyegon",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii niweze kuchangia Hoja hii. Culture ni utamaduni na vitu ambavyo watu wa zamani walikuwa wakitumia. Waswahili wanasema ‘Mwacha mila ni mtumwa.’ Mtu ambaye anasahau mila yake na vitu ambavyo watu wake walivitumia hapo zamani, ni mtumwa. Wakati wa ukoloni, wazungu walikuja nchini Kenya na kutembea Barani Africa wakisambaza utamaduni wao na mambo waliokuwa wakifanya kwao na kufanya mila zetu zikae kama si za maana. Waafrika wote walipokea hiyo injili wakati huo na wakaamini kwamba utamaduni na vitu tulivyokuwa tukitumia kitambo havikuwa vya maana. Walituletea Bibilia na tukakubali kubatizwa na kufuata Yesu Kristo. Tukisoma Agano la Kale na kulinganisha utamaduni wa Wayahudi na utamaduni wa Waafrika – na haswa utamaduni wa watu wa Bonde la Ufa – tunaona kwamba tamaduni hizo mbili zinafanana sana. Hivyo basi tukaamini kwamba utamaduni wetu ulikuwa muhimu sana. Na ni vile watu walikuwa wanataka kutuona ama kufanya yetu ikae kama kitu kibaya. Ninaungana na wenzangu kusema kwamba vitu ambavyo… Nimetembea mara mingi sana hadi huko Ulaya nikaingia katika mahali ambayo wanaviweka vitu vyao."
}