GET /api/v0.1/hansard/entries/1323784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1323784,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323784/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
"speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
"speaker": null,
"content": "Nilitembea kwa makavazi huko Ulaya haswa London ama Uingereza. Kwa makavazi zao, wameweka vitu vingi sana vya Kiafrika. Nilishangaa kwa sababu nilienda kuuliza baadhi ya vitu hivyo ni vya nchi gani. Nikaambiwa vingine ni vya Côte d'Ivoire; vingine ni vya Kenya; na vingine sijui ni vya Tanzania. Nilishangaa mbona walikuwa wanakashifu vitu hivyo wakati walikuwa hapa Kenya ilhali wamevipeleka huko kwao wavitumie kama vitu vya kufundisha watoto wao. Siku moja pia tulikuwa na sherehe upande wa Narok. Watu walikuwa wanalalamika sana. Kuna watu ambao waliuwawa wakati wa ukoloni na vitu vyao vikachukuliwa vikapelekwa huko ng’ambo. Miaka sabini ama mia moja baadaye, wazungu fulani wakavipata hivyo vitu wakavirejesha huko nyumbani. Watu walisherehekea sana. Nikatembea pia upande wa Nandi na tukapata ya kwamba kuna mzee alikuwa shujaa aliuwawa anaitwa Koitalel Samoei. Walichukua kichwa na kubeba vitu vyake alivyokuwa akitumia kutafsiri na kuongoza watu; fimbo kama ile ya Yoshua ama ya Musa wakati alikuwa anawaongoza wana wa Israeli. Watu waliwaambia hawa watu warudishe vitu hivyo. Walirudisha vitu hivyo lakini kichwa hawakurudisha. Tungependa tuseme hata sisi Wakipsigis na watu wengine pia tuko na mali yetu ambayo ilichukuliwa na wazungu na tungependa irudishwe, na vitu hivyo vije viwekwe kwenye makavazi yetu ya Kiafrika ama Kenya. Vitu hivyo vipate kuheshimika na pia sisi kama Wakenya tuhakikishe ya kwamba vile vitu ambavyo watu wetu walikuwa wanatumia kwa utamaduni wetu viheshimike. Hakuna utamaduni wa mtu ambao ni mbaya. Tumeona kwa sherehe nyingi... Tukienda sherehe ya kitaifa Meru, tunaona mavazi ya Wameru ni maridadi sana. Tukienda Kiambu, tunaona mavazi ya watu wa Kiambu ni maridadi sana. Tukienda Narok, tunaona mavazi ya watu wa Narok. Hata juzi walianza kitu kinachoitwa siku ya utamaduni yenye wanasherehekea utamaduni wao na mavazi ya watu hao. Sisi pia watu wa Bonde la Ufa tumesema lazima tuweke siku yetu ya kitamaduni ndiposa ile mavazi ambayo akina mama na babu zetu walikuwa wanavaa hata wakati wa kutahiri, mambo hayo yote yarudi tufundishe watoto wetu. Hivyo vitu vilikuwa vinafundisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}