GET /api/v0.1/hansard/entries/1323797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1323797,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323797/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "tulikuwa zamani tukitumia jiwe la kusaga. Hizo kwetu ziko mpaka sasa. Hapa Kenya jamii nyingi zinazo lakini hazionyeshi ni kama ni kitu muhimu. Kule kwao wanachukulia umuhimu wa vile vitu. Wameviweka kwenye nyumba nzuri, makavazi mazuri, ziko kwenye glesi na zinapendeza na watu wengi wanaenda kuangalia zikivutia uchumi. Sasa zile zetu zimechukuliwa huku wakaenda wakazipeleka kule zinawapatia pesa. Ni muhimu nazo zirudi na sisi nasi tuviweke vizuri na zile ambazo tuko nazo hazijaenda nje pia nazo tuziweke vizuri. Kila jamii ina tamaduni zake na zile tamaduni tunaona vitu vidogo vidogo tunaweza kuviweka watu wakaja na kusudi la kuviangalia vitu kama hivyo na vikaleta watalii wengi. Kwetu, kule Lamu Mashariki Kisiwa cha Pate ni kisiwa chenye historia kubwa ya kitamaduni. Ni sisi tu Serikali hatujafuatilia zaidi. Kule kuna nyumba ambazo sisi tunaziita magofu ya kutoka kabla wakati wa Mtume Mohammed hajaambiwa tuabudu tukiswali tukielekea Makkah. Kuna msikiti kwenye kijiji kinachoitwa Shanga. Kuna ile qibla . Qibla ni pale Waislamu wanaangalia wakiswali. Kwenye qibla hii, walikuwa wanaangalia Jerusalem. Saa hii ukiangalia hicho qibla, ukiweka compass, inakuonyesha unaangalia Msikiti Al-Aqsa. Kisha baadaye, Mtume Sallallahu Aleyhi Wasallam aliambiwa abadilishe kutoka huko, iende Makkah. Historia kama hizo ziko humu ndani na zinaozea pale. Sisi Wakenya hatufanyi bidii tukazionyesha na watu wakajua kama vile watu wanavyokuja Maasai Mara kuangalia hao nyumbu. Hatuzifanyii kazi kisha wengine wakichukua ndio tunalalamika. Hakuna kaunti ambayo haina mambo ya kitamaduni. Katika mambo mengine ya kitamaduni, ni sharti sisi wenyewe tukuze utamaduni wetu. Tuhakikishe angalau sherehe hii ya utamaduni inazunguka kama ilivyokuwa zamani. Kama safari hii ni Lamu, wakati mwingine twende kwingine ili utamaduni ujulikane. Lazima tuukuze utamaduni watu wajue ili pesa ziingie. Watoto wetu na vizazi vyetu vijue utamaduni wao. Tumewacha utamaduni na watoto wetu wanaingia kwenye mambo kama ya mihadarati. Kama kwangu, utamaduni hakuna. Zamani tulikuwa tukipiga maulidi, tukifanya zile kwetu tunaita sorio, na mambo mengi ya kitamaduni. Sasa hivi, hakuna utamaduni huo. Tunasema disko ni mbaya, lakini wao wanaenda huko. Tunasema mihadarati ni mibaya, na wao wanaenda huko, kwa sababu hakuna mambo kama yale ya kitamaduni ya kumshika yule mtoto. Kwa mfano, zamani kabla msichana hajaolewa, alikuwa akiitwa aende kwa wazee waliokuwa wanamfunza mambo mengi. Siku hizi, watu wanaolewa bila kujua chochote na ndoa zinavunjika. Zote zinasababishwa na sisi kutofuata ule utamadani wetu."
}