GET /api/v0.1/hansard/entries/1323831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1323831,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323831/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Masinga, Independent",
"speaker_title": "Hon. Joshua Mwalyo",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana ndugu yangu Mheshimiwa KJ kwa kunikosoa na kunieleza zaidi. Lakini, niko na miaka mingi kidogo tangu nizaliwe. Nilikuta Wakamba tu ndio walikuwa wakitengeneza hivi vitu. Wale wengine wamejifundisha kutoka kwa Wakamba. Kwa hivyo, wacha niendelee tu. Kitu cha maana ni sisi wenyewe tuhifadhi mila yetu ili watu wengine wasiichukue na kusema ni yao. Wanaweza kuchukua utamaduni wetu kuwa kama mali yao na waseme ni wao walivumbua na kuanzisha huu utamaduni. Kisha wataununua hata kwa fedha ndio uwe wao. Hii ndiyo inasemekana tukatae na sisi tumiliki kile ambacho ni chetu na tukatae nacho. Pamoja na hayo, kuna mambo mengi sikubaliani nayo. Mfano ni vile wengine wanasema turudi kwa mila zetu. Mimi siwezi kukubali tuanze kuomba kulingana na mila zetu kama tulivyokuwa tunaomba Mlima Kenya. Ati tuondoke kwa kumwomba Mungu wa asili na tuanze kuomba vitu vingine ambavyo si vya ukweli. Siwezi kurudi kwa desturi ya Wakamba ya kuroga watu iitwayo kamuti . Mtu angekuroga na kila angesema kingetendeka. Dunia inaendela mbele na watoto wetu wanasoma ili waendelee mbele. Tusijirudishe kule."
}