GET /api/v0.1/hansard/entries/1323835/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1323835,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323835/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dagoretti South, UDA",
    "speaker_title": "Hon. John Kiarie",
    "speaker": null,
    "content": " Mheshimiwa Spika wa Muda, ni vizuri kwamba Mheshimiwa Mwalyo ametusisimua na hoja yake hii ambayo anaileta. Lakini ningependa nimwarifu Mheshimiwa Mwalyo kwamba ingekuwa vyema amsome msomi anayejulikana kama Professor Mailu ili afahamu tamaduni hizi za Wakamba. Jambo hili analotaja kujulikana kama kamuti analiita urogi. Angekuwa amefahamu tamaduni za kikamba vyema, angeelewa kwamba hatufai kujidharau wanapotudharau. Ujuzi wetu wa kisayansi na kiteknolojia utaitwa urogi hapa nchini. Wakienda kule uzunguni ama ughaibuni, wanauita teknolojia, metaphysics au spirituality. Lakini kwa mila zetu, vitu ambavyo vinafaidi watu wetu kama vile kuweza kuungana na Mungu wetu na pepo za waliotuwacha tunaviita urogi. Ningependa nimkosoe kwa kumjulisha kwamba hatutakubali tudharauliwe wanapotudharau kule nje. Ingekuwa vyema afahamu hilo."
}