GET /api/v0.1/hansard/entries/1323846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1323846,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323846/?format=api",
    "text_counter": 174,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sotik, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Francis Sigei",
    "speaker": null,
    "content": " Mheshimiwa Spika wa Muda, mimi pia ningependa kuchangia Hoja hii kwa lugha ya Kiswahili. Nimechukulia siku hii ya majadiliano kama siku ya maana kwa sababu imetuletea maswala mawili. Mhe. Spika wa Muda, la kwanza, inatuambia kuwa ni lazima Serikali ifikirie jinsi ya kuimarisha lugha ya Kiswahili kwa sababu ni lugha ya maana. Ningependa hata Bunge hili letu tuanze kufikiria nguo ya Kitaifa ya kuvaa hata siku moja. Niliona Wabunge wengine, hasa akina mama, walivaa nguo ya kitamaduni. Wanaume pia tungependa kuweka kando siku ambayo tutavaa nguo za kitamaduni."
}