GET /api/v0.1/hansard/entries/1323855/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1323855,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323855/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitui Kusini, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Dr) Rachael Nyamai",
    "speaker": null,
    "content": "Ninapounga mkono Hoja hii, Wakenya - hasa Wamaasai - wana nguo nzuri sana ambayo ni ile shuka ya Kimaasai. Nimeangalia katika mtandao na nimeona kwamba hata sasa hivi, huwezi jua ni ya nchi gani. Imechukuliwa na nchi zingine na wanajivunia. Pia, wamesajili hilo jina, shuka la Kimaasai. Sasa, hujui kama ni ya Kenya ama ni ya wapi. Kwa hivyo, tunafaa kujivunia utamaduni na nguo zetu ambazo tulikuwa tunavaa. Nimeangalia vile Wakamba walikuwa wanavaa nguo nzuri sana zamani. Sio lazima twende kazini na nguo hizi. Tunaweza kujitokeza siku moja na tuzivae. Wasichana wetu, hasa wale wanafanya Mtaala Unaozingatia Uwezo, hali maarufu CBC, wanaweza kuvaa hizo nguo na watuonyeshe vile wasichana wetu wa Kikamba, Kimaasai au Kisamburu walikuwa wanavaa. Nitatumia fursa hii pia kukubaliana na mtindo wa CBC, kwa sababu unaonyesha watoto wetu vile ilivyokuwa na pia kujaribu kufurahia vile tulikuwa tunavaa nguo na kuimba. Pia, nimechukua muda nikaangalia kiondo . Mhe. KJ ambaye tulisoma pamoja ataniambia kama ni jina la Kiswahili. Lakini, limechukuliwa na Wachina na watu wa Kijapani."
}