GET /api/v0.1/hansard/entries/1323864/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1323864,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323864/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui Kusini, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Dr) Rachael Nyamai",
"speaker": null,
"content": "Ni kikapu ambacho tunajivunia na kukiuza. Tujaribu iwezekanavyo kukataa nacho ili kisiwe cha Wachina au Wajapani kwa sababu wamekichukuwa na kikawa chao. Nimekuwa nikienda mikutano ofisini mwa Mheshimiwa Sarah Korere, ambaye huwa anavalia vizuri na kujipamba mapambo mazuri mazuri. Sijui kama Mheshimiwa huyo ni Mndorobo, Msamburu au Mmaasai. Huwa anavutia sana anapovaa nguo za kikwao. Sijui kama Kamati hii inaweza kutusaidia kuandikisha mavazi yetu yawe ni ya Kikenya. Dunia imekuwa kama nchi moja kubwa. Tunajivunia kuona watu kutoka sehemu tofauti, wakiwemo wazungu, wakijivunia mavazi yetu. Tunajua kuwa kuna watalii ambao wanaweza kubeba ngozi za wanyama wetu mifukoni mwao bila jambo hilo kujulikana. Jambo hilo limefanyika. Juzi tu, tuliona mtu ambaye alikuwa amebeba vifaa tofauti tofauti katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Tunawaenzi polisi wetu kwa kukamata vitu hivyo. Ni vizuri tujivunie wanyama wetu ambao wanatuletea watalii wengi. Tujivunie pia mavazi, nyimbo na lugha yetu ya Kiswahili, ambayo hatujaimudu kabisa, lakini tulisomeshwa na kwa sababu hiyo, tutatia bidii kuizungumza ipasavyo. Ninapomalizia, ningependa kuchukua fursa hii kumuenzi rafiki yangu, Mheshimiwa Kiarie John, aliyeeneza mambo ya utamaduni akiwa kijana mdogo sana. Alikuwa mdogo wangu shuleni. Alieneza utamaduni katika mchezo wa kuigiza uliokuwa ukiitwa Redykyulass, na alitengeneza pesa nyingi akawa kama mwalimu wa chuo kikuu wala sio mwanafunzi. Ninamuenzi sana kwa sababu mchezo huo wa kuigiza pia ulikuwa ni utamaduni ambao umeendelezwa na vijana wetu leo. Wameusukuma mbele ukawa kiwanda kizima katika biashara."
}