GET /api/v0.1/hansard/entries/1323875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1323875,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1323875/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nichangie Hoja hii ambayo imeletwa na Kamati ya Michezo na Utamaduni. Mswahili anatuambia kuwa mwacha mila ni mtumwa. Tukiwacha mila zetu na tukubali mila ambazo tuliletewa, tutakuwa watumwa katika njia moja au nyingine. Sisi kama Wakenya, haswa Wameru, tumekuwa na mila na uhusiano wa karibu sana. Mila tulizolelewa nazo ni za kujiheshimu na kuwaheshimu wazee wetu. Kuwacha mila kama hizo ni kupotea njia. Katika utamaduni wetu wa Kimeru, Mmeru hangekubaliwa kuoa kama hajaleta miraa. Sijui kama kuna mahali pengine duniani ambapo ndoa hairuhusiwi kwa ajili ya sababu kama hiyo. Ningependa mila na tamaduni zetu zifuatwe, zilindwe na kutunzwa ili kijana wangu akioa Uarabuni, itanibidi nipeleke miraa huko. Hiyo ingethibitisha wazi kuwa utamaduni wetu unaaminika. Tuenzi tamaduni zetu na lugha yetu ya Kiswahili. Kwa sababu Kiswahili ni lugha inayokuwa, hata neno “ kiondo” linatumika na kukubalika katika lugha ya Kiswahili."
}