GET /api/v0.1/hansard/entries/1324610/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1324610,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1324610/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, pia najiunga na Kiongozi wa Wengi kupongeza Kamati ya Sheria na Haki ya Bunge la Seneti kwa kazi nzuri ambayo imefanya. Kusoma ardhilhali tatu kwa muda mfupi uliowekwa wa siku 60, ni kazi kubwa ambayo imefanywa na Kamati hiyo. Sisi wote tunaipongeza. Pia nimesimama kwa masikitiko kwamba mwezi wa saba nilileta maombi ya taarifa kuhusiana na ukosefu wa huduma za lift na hali ya usafi katika Jumba la Bima, Mjini Mombasa. Kuna pia Taarifa kuhusiana na zabuni zilizotolewa na mashirika ya Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) na Kenya Urban Roads Authority (KURA) kwa mji wa Mombasa, miaka kumi iliyopita. Bw. Spika, Taarifa hizo zilipelekwa kwa Kamati ya Usafiri na Miundo Msingi, lakini, masikitiko ni kwamba mpaka leo, zaidi ya miezi mitano iliyopita, sijapata ripoti yeyote kuhusiana na Taarifa hizo. Sijui Kamati imezembea ama imelala kuhusiana na maswala haya. Lile jumba la Bima lina wizara karibu tatu za Kaunti ya Mombasa. Inabidi Mawaziri wapande kwa miguu, karibu gorofa saba au nane. Masoroveya wako gorofa ya kumi na mbili na wananchi wanaohitaji huduma za serikali za usoroveya wanapata shida. Hilo jumba halina maji na lina gorofa kuma na nne. Bw. Spika, ningeomba utupe mwongozo wako kuhusiana na swala hili. Hili ni jambo linakera roho wakaazi wa Mombasa. Asante."
}