GET /api/v0.1/hansard/entries/1324615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1324615,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1324615/?format=api",
"text_counter": 44,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, malalamiko yangu ni kwamba mnamo mwezi wa saba, niliomba Taarifa kuhusiana na maswala mawili. Ya kwanza ni ukosefu wa huduma ya lifti katika Jumba la Bima Towers mjini Mombasa. Jumba hili lina gorofa kuma na nne na linahudumia wananchi kuhusiana na maswala ya usoroveya. Kuna pia Wizara tatu za Baraza la Kaunti ya Mombasa zinazohudumu ndani ya jumba hili."
}