GET /api/v0.1/hansard/entries/1324618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1324618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1324618/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, niliomba Taarifa kuhusiana na ukosefu wa huduma za maji na lifti katika jumba la Bima Towers, Kaunti ya Mombasa. Jumba hili lina wizara karibu tatu za Serikali ya Kaunti za Mombasa ambazo wananchi huenda kutafuta huduma huko. Maji hupelekwa na mkokoteni huko na hiyo ni kinyume na matarajio ya wengi katika Kaunti ya Mombasa. Taarifa ya pili niliyoomba ni orodha ya zabuni zilizotolewa na mashirika ya KeRRA na KURA katika Kaunti ya Mombasa kwa muda wa miaka kumi ya ugatuzi. Hii ni kwa sababu kuna kero kwamba hakuna barabara zinafadhiliwa na mashirika haya mawili ya KeRRA na KURA katika Kaunti ya Mombasa. Bw. Spika, hayo ndiyo maombi yangu ya Taarifa niliwasilisha mwezi wa saba mwaka huu. Asante."
}