GET /api/v0.1/hansard/entries/1326334/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1326334,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326334/?format=api",
"text_counter": 80,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": "Bw. Spika, nilikuwa natarajia kumwona Waziri wa Kawi, Mhe. Chirchir kwa sababu watu wa Tana River wanajua Kenya Electricity Transmission Company (KETRACO) walilipwa pesa ili zile nyaya zao zipite kwa mashamba za watu. Watu wanajua mamilioni ya pesa zililipwa lakini wananchi hawakupata hizo pesa. Wananchi wa Tana River wanangoja kuelezwa hizo pesa ziko wapi, halafu, Waziri anakosa kuja ilhali wananchi wanamngoja. Bw. Spika, ningependa kutoa maoni yangu ya kwamba utoe faini sio ya elfu mia tano lakini faini ya milioni moja kwa kila waziri ambaye anakosa kufika kwa Bunge la Seneti. Kisha uandike barua kwa Rais kwamba wakati wa kufuta kazi Mawaziri, wa kwanza kufutwa ni hawa Mawaziri ambao wanakosa kufika Seneti kujibu maswali ya wananchi. Bw. Spika, kwa hayo mengi naomba uchukue mkono wako wa nguvu uwatie hawa watu adabu kwa sababu wanatukosea heshima. Asante, Bw. Spika."
}