GET /api/v0.1/hansard/entries/1326341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1326341,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326341/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, Mawaziri husika wameonyesha kwamba hawana heshima yeyote na Seneti. Mawaziri hao walianza kwa kukejeli na kudhihaki Kamati zetu. Wakiitwa katika Kamati, hawakuji na hata hawasemi chochote. Sasa wameona kwamba wamehitimu. Kutoka kwa kamati, sasa wanataka kukujaribu wewe kama Spika wa Seneti. Wanangoja kwa hamu na ghamu waone utafanya nini. Usipofaya jambo leo, Seneti itakuwa imezama lakini mimi nina imani ya kwamba wewe kama Spika wetu utafanya jambo. Nilikuja hapa asubuhi na mapema ili niweze kuona Waziri wa Kawi anieleze ni mipango gani aliyonayo kwa sababu sehemu nyingi za Kaunti ya Laikipia hazina stima kwa sababu ya maji. Nilitaka kujua ni mipango gani alizonazo. Sababu tunazopewa sio za kutosha. Hata kuna Waziri aliyekuambia asubuhi ya kwamba, yeye alikuwa na mipango mingine maalum. Katiba ya Kenya katika Kipengee cha kwanza inasema, nguvu zina wananchi wa Kenya. Sisi ndio tunawakilisha wananchi wa Kenya. Ninangoja kwa hamu kuona maamuzi yako. Namshukuru Sen. Thang'wa, ambaye ni mojawapo wa wenyeviti wa Kamati za Seneti. Jana alifanya jambo na Wakenya wakaona amefanya jambo la maana. Waswahili husema, kizaliwacho ni kizuri kuliko kinachozaa. Ninangoja ."
}