GET /api/v0.1/hansard/entries/1326419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1326419,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326419/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kuna baadhi ya mambo ambayo bado yanaendelea katika maswala ya Shakahola. Kwa mfano, kuna wale ambao walichukuliwa kama manusura katika ile sehemu Pastor Mackenzie alikuwa anahudumu. Wale walichukuliwa sio wale waliyofanya mauaji au vitendo vya kinyama, lakini waathiriwa ambao walipatikana pale. Mpaka sasa, waathiriwa hawa bado wako Shimo la Tewa. Wamewekwa pale kama hifadhi. Mnamo Mwezi wa Nane kabla kupelekwa katika gereza la Shimo la Tewa, walikuwa wamepewa hifadhi katika shule moja ya kibinafsi pale Mtwapa. Tarehe 12 Agosti, 2023, walikuwa wamepanga kujiuwa wote pamoja. Lakini, baadhi yao walitoa hizi habari na maafisa wa usalama wakawachukuwa wote wakawapeleka katika gereza la Shimo la Tewa ambako bado wanaendelea kufanyiwa uchunguzi na ushauri nasaha, yaani, counseling, ili kuhakikisha kwamba zile fikira walizokuwa nazo za kujitoa uhai ziondoke katika fikira zao. Bw. Naibu Spika, tunapongeza mahakama, hususan Mahakama ya Shanzu ambayo baadhi ya washukiwa wamewekwa na wanaenda kortini mara kwa mara, ili kuitikiwa au kuangaliwa ni vipi wanaweza kusaidika ili warejee katika jamii."
}