GET /api/v0.1/hansard/entries/1326427/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1326427,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326427/?format=api",
    "text_counter": 173,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mahakama imefanya kazi nzuri hadi sasa . Ijapokuwa, mahakama za awali zilimpa Pastor Mackenzie uhuru mwingi usiostahili kupewa kulingana na maswala ambayo yalikuwa yanachunguzwa wakati ule. Tumeona pia kuna watu wengi waliyohusika katika maswala ya Shakahola, wale ambao tunaita First Responders kwa Kiingereza, kama vile; Kenya Red Cross, yale mashirika ya haki za kibinadamu, polisi na watu wa upausaji; almaarufu pathologist. Wamefanya kazi nzuri kabisa kusaidia jamii na waathiriwa kupata nafuu na ushauri kutokana na majanga yaliyowakumba. Red Cross wametoa mchango mkubwa. Wale walioenda kule kwanza, hakukuwa na mfumo wowote uliyowekwa. Lakini kwa uwezo wa Redcross, waliweza kuchangia pakubwa. Mpaka sasa, ile miili ambayo imewekwa kule Malindi Mortuary, imewekwa katika hifadhi ya Red Cross. Wametoa container ambayo imewekwa barafu na miili yote imewekwa pale. Jambo la kusikitisha ni kwamba licha ya kwamba tulikuwa na janga la COVID-19 miaka miwili na nusu iliyopita, Serikali ya Kilifi haikujitayarisha kuwa na hifadhi ya kutosha kuweza kuweka miili mingi, kama walivyo tarajiwa kufanya walipopewa pesa za COVID-19 mwaka wa 2021. Bw. Naibu Spika, ni lazima kaunti zetu ziwe na uwezo fulani wa kujitayarisha. Haiwezekani janga kama hili limetokea Kaunti ya Kilifi na hatuna uwezo wa kuhifadhi miili ya walioathiriwa. Ninakubaliana na mapendekezo yote kwamba ni lazima uchunguzi ufanywe. Tumeona Waziri wa Usalama wa Ndani, Mhe. (Prof.) Kithure Kindiki alizuia baadhi ya mashahidi kuenda kutoa ushahidi. Alimzuia Waziri Aisha Jumwa kuja kutoa Ushahidi wakati Mhe. Aisha Jumwa alikua mtu wa kwanza kuonyesha bendera nyekundu kuhusiana na maswala ambayo yalikua---"
}