GET /api/v0.1/hansard/entries/1326466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1326466,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326466/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "ilikua imepungua. Mikataba mingi wamefanya na mashirika yanaleta vile vifaa kame yale mahabara yanayotumika kuchunguza mambo mengi, imekwisha na pesa hazijalipwa. Bw. Naibu Spika, ipo haja ya Serikali, sababu DCI inafanya uchunguzi wa maswala ya jinai na uhalifu. Ni shirika muhimu katika nchi yetu kwa hivyo, lazima iweze kupata pesa za kutosha ili izuie maafa kama haya ya Shakahola na mengine ambayo yanaweza kutokea katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika, naunga mkono Ripoti hii. Ningependa kwamza Seneti iweze kuzikubali zile taasisi ambazo zimeombwa ziweze kuifanyia kazi, tuone kwamba mashirika ya kidini ambayo yana taswishi na yanafanya mambo kinyume cha sheria, maadili na vitabu vya Mwenyezi Mungu, yameweza kusimamishwa ili wananchi waishi kwa usalama."
}