GET /api/v0.1/hansard/entries/1326615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1326615,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326615/?format=api",
    "text_counter": 361,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Nisamehe kidogo, hali yangu ya afya kidogo iko na tatizo kwa hivyo sauti yangu haiko sawa. Nina mafua ya mvua ya El Nino na kadhalika. Kwanza, natoa kongole kwa kamati yetu ambayo tulituma kwenda kufanya hii kazi ya kuchunguza maafa yaliyotokea huko Shakahola katika Kaunti yangu ya Kilifi, ninayowakilisha katika Seneti. Kamati hii ilifanya kazi ngumu sana. Kazi ya kusikitisha lakini ilikuwa ni sharti waifanye kulingana na yale maafa yaliyotokea. Nampa kongole aliyekuwa Mwenyekiti, Sen. Mungatana na kamati yake kwa kazi waliyoifanya. Jambo la pili, mimi kama Seneta wa Kilifi, vile nivyofanya kazi katika mahakama ya Kenya na Kiongozi wa Walio Wachache katika Seneti hii, nakemea sana wale watu waliokataa kuhojiwa na kamati hii. Katika kazi ngumu iliyofanyika, kuna watu waliotakiwa kuhojiwa na hii kamati. Lakini wengine wao waliambiwa wasiende na wengine, wakajipa shughuli ili wasiweze kufika mbele ya kamati hii. Bw. Spika wa Muda, kamati ya Bunge ni kamati muhimu sana. Ikiwa haswa kamati hiyo imeundwa na Bunge, ni lazima iheshimiwe. Tumeona kwamba kuna watu fulani wenye mamlaka Serikalini, wanawaambia mashahidi fulani wasiweze kufika mbele ya kamati hii. Hili ni jambo ya kusikitisha. Kule Shakahola, miili mingi ilipatikana ikiwa imetupwa ama imefukiwa huko. Shughuli kubwa sasa ilikuwa ni kuwafukua. Wengi wa wale watu ni watu ambao hawakutoka katika ile sehemu ya Shakahola. Hili lilikuwa na tukio la kusikitisha sana."
}