GET /api/v0.1/hansard/entries/1326617/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1326617,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1326617/?format=api",
    "text_counter": 363,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Watu hawa walifanyiwa maafa wakiwa mbali na nyumbani mwao. Walikuwa wametoka maeneo kama vile kaunti za Magharibi, kaunti kama Kakamega, vile Sen. (Dr.) Khalwale alivyokubaliana, na pande zote katika nchi ya Kenya. Ni kama kulikuwa na mipango maalum kwa sababu hawa ni watu ambao waliuliwa huko. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba, tuko na Serikali na mpaka wa leo, haikuweza hata kidogo kutambua wale watu waliowaua wengine. Hao watu waliwaua na kusafirisha miili zaidi ya 500 kutokea pande zote za Kenya hadi Kilifi County, Shakahola kuwazika huko. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba leo tunasema, tuko na Serikali. Ni Serikali gani mbayo inaweza kuona maafa ya namna hiyo yakitendeka humu nchini na iwe haijui ama haiwezi sema hao watu waliuawa wapi na ilikuwa namna gani mpaka wakapatikana sehemu za Shakahola. Hilo ni jambo la kusikitisha sana. Bw. Spika wa Muda, tumekuwa na maafa katika Mkoa wa Pwani, kuanzia Lunga Lunga mpaka Kismayu. Watoto wetu wa kiume wamekuwa wakipotea kutokea manyumbani. Ukienda Old Town saa hizi, kuna wajane wa wasichana wadogo na kina mama. Ukienda maeneo mbalimbali ya Kilifi, kuna wajane wa vijana barubaru waliokuwa wakiishi na wakifanya kazi zao. Mpaka leo, miili hiyo haijapatikana kutoka wapotee katika mikono ya polisi. Pia miili hii haijapatikana. Ni kumaanisha ya kwamba, uchunguzi ufanywe katika ile miili iliyofukuliwa kiaibu kule Shakahola. Inaweza kuwa watoto wetu waliopotea. Ikiwa ni Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamu na Taita Taveta, kwa wale watoto wetu wote waliopotea. Pengine tunajua wengine ni hao walio hapo Shakahola. Jambo ninalotaka hii kamati iweze kupendekeza au iongeze ni ya kwamba wale wazazi wa Kiislamu na Kikristo waliopoteza watoto wao, wapeane Deoxyribonucleicacid (DNA) zao ili zichukuliwe na zipimwe na ile miili iliyohifadhiwa kule Malindi na Dr. Oduor. Ili huyu daktari atambue na aseme kama kuna wale watoto wetu waliopotea. Ili pia tuweze kujua na kuregeshewa ile miili ya watoto wetu ndio tuwazike na tujue kwamba wamepatikana. Sasa tunawazika tukijua hatutawaona tena, kuliko kujua walipotea katika mikono ya polisi na hatukuchukua hatua yeyote sisi wenyewe. Serikali ambayo sisi husema tuko nayo, haikufanya lolote, ilihali, Katiba inasema maisha yanalindwa na Serikali Bw. Spika wa Muda, vilevile, sisi watu wa Kilifi Kaunti ni watu wakarimu sana. Tumeletewa aibu ya kitaifa ambayo hatujaiona na ndiyo sababu nilikataa kuketi kwa hiyo kamati. Kwa sababu, aibu kama hii imetendeka na vile vigogo vya polisi bado vipo Kilifi. Bw. Spika wa Muda, ukiniruhusu, ninaweza kukuelekeza ukurasa wa 425 iliyo na wale wakuu wa polisi waliotajwa hapa. Kuna Joseph Kemboi, aliyekuwa SeniorSuperintendent of Police, Charles Kamau Wanguhu, Assistant Superintendent of Police, Malindi, Solomon Odera, Superintendent of Police, Sub-County Police Commander, Agamso Guracha, Superintendent of Police, Critical Infrastructure Protection Unit, Augusto Okumu, Officer Commanding Station, Malindi, Hassan Habara, OfficerCommanding Station, Lango Baya na Calvin Maloa Otieno, Directorate of CriminalInvestigations – mtu wa mambo ya jinai hapo Malindi. Pia, kulikua na Daniel Muthusi Muleli, County Criminal Investigation Officer,"
}