GET /api/v0.1/hansard/entries/1336643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1336643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1336643/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": "Taarifa ambayo imesomwa katika Bunge hili ni uongo mtupu. Hata namhurumia Mheshimiwa aliyesoma Taarifa hiyo kwa sababu ni kama hajui wanawake na wasichana wanapata hedhi miezi mingapi kwa mwaka. Kwa hivyo, ni mambo ambayo yeye mwenyewe hayajui. Taarifa hiyo ni ya uongo mtupu. Hakuna sanitary towels ambazo zimepeanwa kwa mashule kwa muda wa mwaka moja. Walimu wako hapa na wanashtuka. Ni aibu kubwa sana. Mhe. Naibu Spika, tuko na shida ya sodo katika nchi yetu na ni lazima iangaliwe na Wizara husika. Mimi ni Mhe. Liza Chelule. Nimechaguliwa kutoka katika Kaunti ya Nakuru. Ninawakilisha akina mama na wasichana wengi. Wasichana wetu wako na shida sana kwa sababu wengi wao hawaendi shuleni kwa sababu wamekosa sodo. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Kauli hii. Mabadiliko katika hali ya hewa yameleta shida kwa mzunguko wa hedhi kwa wasichana wetu. Kwa mfano, msichana atapata hedhi mara tatu kwa mwezi kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya hewa. Katika hali kama hiyo, pakiti sita au saba hazitoshi. Ahsante, Mhe. Naibu Spika."
}