GET /api/v0.1/hansard/entries/1336683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1336683,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1336683/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "hawa wapewe nafasi hiyo ya kupeleka hizo sodo kwa shule zetu za upili na msingi mia kwa mia. Pili, ni uongo sana kwamba wamekuwa wakipeana hizo sodo. Juzi nimekuwa kwetu kule Taita Taveta katika shule ya upili ya Senior Chief Mwangeka Girls. Niliuliza wanafunzi kama wanapata sodo, wakanijibu kwamba hawajawahi pata kwa miaka mitatu. Ni uongo, hazijafikia shule zetu na ni lazima zipatiwe mama wetu hawa waweze kupeleka sodo hizo. Mwisho, vile vile, katika kila zahanati, ukienda utapata mipira ya kondomu. Na ukienda kila mahali katika mahoteli, utapata mipira hio inapeanwa bure. Lazima tupitishe Mswada ndani ya Bunge hili ili sodo hizi zipeanwe bila malipo. Kila mahali kuna public facility, sodo ziwe na zipeanwe bila malipo. Wasichana wetu wanataabika sana. Ahsante sana."
}