GET /api/v0.1/hansard/entries/1337057/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337057,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337057/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ". Zinapotupwa waziwazi, kuna watu huziokota na kuzitumia hata katika hospitali zetu. Ninafikiri tumekuwa na hawa ndugu zetu wa Kenya Medical Supply Agency (KEMSA) jana. Tulikuwa tunawauliza maswali. Ilibainika kuwa kuna dawa ambazo zilipelekwa Kaunti ya Mombasa. Zilikuwa zimebaki miezi miwili au mitatu ziharibike. Mtu wa pharmacy ndani ya hospitali anaweza kuzitoa kumbe muda wa kutumika umepita. Hizi zitaleta madhara zikipewa mgonjwa. Kwa hivyo, tuangalie sheria ambayo itadhibiti na kuhakikisha dawa yoyote isiingie Kenya ikiwa muda wake wa kuisha uko karibu. Dawa hizi zisitishwe katika mipaka yetu. Tumekuwa akina mama wa kuenda na kubisha chemists kwa sababu mtoto anakohoa kisha tunachukua dawa yoyote. Kuna dawa nyingi zisizofaa zilizotengenezwa katika mataifa ya nje. Kwa mfano, kulikuwa na tetesi kuwa kuna dawa zilizotoka Pakistan na India. Tuliona picha zilizoonyesha kuwa wanazitengenezea nyumbani. Hizo dawa zimepata njia ya kuingia katika taifa letu na kuleta madhara. Kwa hivyo, ninaunga mjadala huu mkono. Ninaafikiana na hii Kamati. Ninawapongeza kwa kusema lazima tuweke sheria ambayo itakayodhibiti sekta hii ya dawa. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}