GET /api/v0.1/hansard/entries/1337064/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337064,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337064/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ninakushukuru Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi kupenyeza sauti yangu, ingawa nilikuja mapema nikitaka kuzungumzia mambo ya ajali barabarani lakini sikupata nafasi. Ninaipongeza Kamati kwa kuja na kanuni za kulinda afya za wananchi, kwa sababu taifa lenye nguvu ni lile ambalo wananchi wake wana afya. Ni vyema sana wale wanaouza madawa wawe ni watu ambao wana ujuzi huo, sio tu wanapeana. Hii ni kwa sababu mara nyingi, daktari anapoandika madawa, wanarudi wanasema: ‘Hizi hakuna, lakini hizi zinafanana.’ Kwa hivyo, zingine zinadhuru wananchi. Pia, wananchi wanafaa waelezwe kwa makini kwamba, ‘dawa hii unatumia madhara yake ni haya.’ Dawa nyingi ziko na side effects . Mtu anaanza kutibiwa ugonjwa huu, mara anaambiwa figo tayari imeharibika. Kwa hivyo, ni vyema sana watu wawe na taarifa kamili ya kiwango cha madhara ya hayo madawa. Kwa hivyo…"
}