GET /api/v0.1/hansard/entries/1337129/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337129,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337129/?format=api",
"text_counter": 56,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika, nimechanganya makabila tofauti. Babangu ni Mmijikenda. Mamangu ni Mbaluhya. Nimeolewa na Msame-Mzaramu. Nimechanganya lakini haitakuwa sawa ikiwa leo mimi nitaambiwa “toka hapa, nenda kwenu” ama iwe hivi na vile. Sote ni Wakenya. Tunafaa kukaa mahali popote. Hata hivyo, nitasema kwamba historical land injustices zimekuwa sababu ya vita vingi kutokea ndani ya Pwani. Ningeomba Wapwani wote watritiwe kwa njia moja. Kama ni maswala ya mashamba, Wabajuni wakipewa titles, wengine wote wapewa titles ili kubalance . Matatizo yanatokea kwa kuwa nimezaliwa hapa, hapa ndio nyumbani, na sina cheti huku pengine mwenzangu aliyezaliwa hapa na ni wa kabila lingine amepata cheti. Ikiwa Serikali itachukua Wakenya wote kuwa hadhi moja na sisi Wapwani tupewe hatimiliki za mashamba yetu, tutaweza kutatua haya matatizo."
}