GET /api/v0.1/hansard/entries/1337308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1337308,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337308/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Wengi wakipata ajali, wakikimbia kwenye kampuni za bima, unapata kuna vuta nikuvute: mara gari lilikuwa wapi? Uligongwa nyuma au mbele? Ulikuwa mlevi? Wanaleta masharti mengi ambayo hawaelezei mwanzo ukianza kuchukuwa hiyo bima. Kuna Wakenya wengi ambao hawaelewi sheria na masharti na unapata… Samahani kama kuna ma wakili hapa. Unasikia kampuni ya bima inamwambia nenda ukatafute wakili. Anatafuta wakili wa kumsaidia kwa sababu haelewi na amekuwa akilipa. Pesa zikitoka anapewa kitu kidogo pesa zingine nyingi ambazo zingemsaidia zinaenda kwa wakili kwa sababu naye amefanya kazi. Lakini sasa ingekuwa wanaeleza Wakenya na inakuwa wazi kuwa wewe ulikuwa umefanya kuweka bima, umepata tatizo, wameliona, wanakusaidia kwa wazi na mgao wako wote ambao utawezakukusaidia. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}