GET /api/v0.1/hansard/entries/1337309/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1337309,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337309/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Nilikwama wakati mmoja hospitalini nikiwa mgonjwa hapa hapa nikiwa Bungeni karibu masaa saba nasubiri sijui kumaliziwa uhakiki wa bima yetu ya afya. Nilitamaushwa sana. Naambiwa kuwa napewa kile chombo cha kupima sukari lakini ile mashine naambiwa nikanunue mwenyewe. Sasa nikashindwa napewa bila mashine kwa sababu kampuni ya bima imekataa haishughuliki na kitu kama hicho. Nikauliza: Sasa nichukue hicho chombo niweke kwa stovu nijipime ama nifanyaje? Kwa hivyo, utapata kampuni za bima nyingi zimekuwa zinakosa nidhamu na zimenyanyasa Wakenya miaka mingi sana. Ninapongeza haya marekebisho ya leo ambayo yameletwa ili waweze kushikwa ikiwa wanawezakosea Wakenya. Hizi penalties ambazo wamewekewa zitafanya wawe na nidhamu katika kuhudumia Wakenya. Wale mameneja na wakurugenzi wawe na nidhamu. Ninapongeza kipengee ambacho kimesema Benki Kuu ya Kenya iweze kushika mgao zaidi kutoka kwa kampuni za bima ili yule Mkenya ambaye atakuwa amepata matatizo na pengine hii kampuni ya bima imefilisika ikaanguka, anawezapata fidia. Watu wengi wamepoteza mali yao kampuni za bima zikawa zimefungwa. Hawakuweza kupata fidia na hawakujua wataenda kuuliza nani. Lakini, leo ninafurahi sana kama Mama Mombasa County kuona mwisho wa hawa watu ambao wamekuwa wakiwatapeli Wakenya kwa jina la bima. Kuna kampuni ambazo zimefanya vizuri lakini zingine zimekuwa kitega uchumi kwao. Wanajua kwamba watakusanya mapeni kutoka kwa maskini na matajiri. Lakini, tatizo likitokea wanaleta masharti na ujanja mwingi. Leo hii ninataka kuwambia sheria inatungwa na kurekebishwa katika Bunge la 13. Ule utapeli ambao ulikuwa unaendelea, leo utakoma na Wakenya watapata huduma bora zaidi. Kuna watu ambao wamepoteza nyumba zao ama zimechomeka. Mtu akienda kwa kampuni ya bima wanakuuliza ni nini kilianzisha huo moto, ilikuwa ni stima ama nini? Kabla wafanye uchunguzi mtu analala nje kwa baridi. Huo uchunguzi unachukua miaka mingi na mtu anapata shida kabla hajapata fidia. Wakenya wamehangaika kwa miaka mingi sana. Mimi ninaweza zungumza mpaka kesho, nikiwaangalia watu wa bodaboda. Mtu amekata bima ya kubeba watu na hajaelezwa kwamba hiyo bima hama huna helmet ama ulikuwa mlevi, hawawezi kukupatia fidia. Lazima wapatiwe masharti yote na waelekezwe vizuri. Lakini, hizi kampuni zinachukua pesa tu na wakati wa huduma wanaleta masharti mengi madogo na kuweza kuhepa kuwapatia Wakenya fidia. Hata kampuni za bima ambazo zinatupatia huduma za hospitali, leo nina furaha kwa sababu tutapata huduma bila kusumbuliwa. Wakenya ambao wako kule chini waliochukua bima ya afya, pia watapata huduma bila kusumbuliwa. Ni dhahiri kuwa miaka nenda, miaka rudi, wahudumu wa bima wamekuwa wakiona Wakenya kwa unyonge wao, kuwatapeli, kuwakosesha haki zao za kimsingi, kuchukua pesa na biashara zao. Wakati Mkenya anapatwa na matatizo anaanza kusukumwa na inakuwa mchezo wa kirba goji, goji kirba. Haelewi ashike wapi ama aende kwa nani. Kama sisi wasomi tulishindwa, je yule Mkenya ambaye hana habari na pesa zake zinachukuliwa kila siku? Imekuwa ni mtihani mkubwa. Ninampongeza sana Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi, Mhe. Kimani Ichung’wah, kwa kuleta haya mabadiliko katika sheria, ili kumfaidi Mkenya. Tunajua kampuni za bima zitapata faida cha kwao cha halali lakini, pia Mkenya aweze kufaidika kwa mapeni ambayo ameweka katika bima. Kwa vile kuna wengi ambao wanataka kuzungumza, nitakomea hapo nikisema nina pongeza sana marekebisho ya Mswada wa mambo yanayohusika na bima. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}