GET /api/v0.1/hansard/entries/1337362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337362,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337362/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "kwa urahisi. Bado kuna vijana wanaoishi sehemu zisizo na mtandao wa simu. Kama ni kuwasiliana nao katika mitandao ya kijamii, kuna sehemu ambako network hazishiki. Tunaposema vijana hawa wateuliwe kutoka kwa wards – jambo ambalo ninaunga mkono – itakuwa bado kuna changamoto ya kuona ni vipi vijana wote katika ward zote zaidi ya 1,000 watapata habari kwa wakati mmoja ili waweze kutoa maombi kupitia hawa directors wa vijana katika kila kaunti. Tutafute mbinu ili habari hizo ziwafikie wakati wowote nao wapate nafasi hii. Mbali na marekebisho haya ambayo ni mazuri, yafaa ifike wakati kuwe na utaratibu zaidi wa kuhakikisha vijana wote wanajumuishwa. Isitokee kwamba ni walio mijini tu ndio watapatikana kwa wingi, na hivyo kuchukua nafasi hizi. Pengine itakuwa wale ambao familia zao zina uwezo kwa sababu ndio watakuwa wanapata habari hizi. Isitokee kwamba vijana wengi ambao familia zao hazina uwezo wakose habari hizi, ilhali wana vipawa ambavyo vingeweza kusaidia katika mikutano na maendelezi vijana. Kwa hivyo, ninaunga Mswada huu mkono. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}