GET /api/v0.1/hansard/entries/1337422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337422,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337422/?format=api",
"text_counter": 349,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Nimekaa sana nikisubiri kuchangia Hoja hii muhimu ambayo Mhe. King’ara ameleta. Kama hungenipa nafasi, nina imani kwamba mizimu ya mababu zangu kule Kwale haingeniruhusu kulala leo. Kwa nini? Suala la ardhi na kupeana stakabadhi limeumiza Wakenya sana, hasa watu wa Kaunti ya Kwale. Kumbukumbu tulizo nazo ni kwamba ardhi ya Kwale ilifanyiwa ukaguzi na kupewa hatimiliki miaka ya sabini. Serikali iliyokuwepo wakati ule ikawaambia wenyeji kwamba kilomita mbili kutoka ufuo wa bahari ni mali ya Serikali. Kwa hivyo, hawangepewa. Watu wakapewa hatimiliki nje ya kilomita mbili kutoka ufuo wa bahari. Hatimaye, mabwenyenye waliokuwa ni hao hao Serikali walikuja wakapeana hatimiliki kwa wageni bila kutambua kwamba wenyeji walikuwa wameishi katika ardhi ile au kuwa wenyeji wamepanda miti ya kudumu. Kuna mikorosho, minazi, makaburi, na visima. Kwa sababu wenyeji waliambiwa ile ardhi inatakikana iwe ya Serikali, Serikali ilitumia nafasi hiyo na kupeana ardhi ile. Nikizungumzia upande wa Kaunti ya Kwale kuanzia Likoni mpaka Shimoni, mahoteli ambayo yamejengwa katika fuo za bahari yako katika ardhi ambazo zilipeanwa na Serkali baadaye. Zilipewa mabwenyenye licha ya kuwa wenyeji walikuwa pale. Mpaka sasa, hali hii bado inaendelea. Kuna hizi sehemu zinaitwa kaya kwa sababu wenyeji walikuwa wanahifadhi misitu na wanajua umuhimu wa kuhifadhi mazingira wakati ule. Watu wanachukua labda kaya ni sehemu ya wachawi au matambiko. Ukweli ni kwamba kaya ni sehemu ambazo wazee wetu walijua zilihitajika kuhifadhiwa. Kuna misitu, miti muhimu ya dawa, na mazingira mazuri ya kufanya hivyo. Kuanzia wakati huo wa miaka ya sabini na mbili, wenyeji walisema wataziacha sehemu hizo kwa sababu ni kaya zetu. Pengine wengine walikuwa wanasema wanaenda kwa maombi. Muhimu ni kwamba hizi ni sehemu ambazo zilikuwa misitu na zinahifadhi mazingira. Nikiwa hapa, baada ya miaka arubaini au hamsini iliyopita, kuna mabwenyenye ambao wamekuja eneo bunge langu pale Tiwi na kuwafurusha wazee. Walikuja na hatimiliki kutoka Nairobi, kwamba wao sasa ndio wanamiliki sehemu hizo za kaya. Waliweka ua hata la stima kwa sababu hawa sio watu wa kawaida katika eneo nzima la kaya. Sasa wao wana hatimiliki. Hili linawanyima watu kutumia rasilimali hii. Wazee hawawezi kuenda. Mabwenyenye hawa wameanza kuleta uchafuzi wa mazingira kwani wameanza kukata ile miti bila kufikiria hili ni eneo ambalo wenyeji walitenga kwa hifadhi mazingira wakati ule hatimiliki zikipeanwa miaka ya sabini. Kuna sehemu ambazo kaya zimeweza kutolewa na hatimiliki kupewa mtu binafsi ili aweze kumiliki sehemu hizi licha ya kwamba hatimiliki zikitolewa, wakaazi waliziacha kwa matumizi ya pamoja. Wakati sheria hii itakubalika na kutiwa kidole inavyostahili, tatizo kama hili halitatokea. Ninamshukuru sana Mhe. King’ara kwa kuleta Mswada huu ijapokuwa umechelewa. Pengine tukiambatanisha na miswada mingine ya kuangalia suala zima la dhuluma za kihistoria, na sheria hii ikipita, ninafikiri suluhu itapatikana. Katika mjadala huu, kuna suala ambalo ni muhimu na limezungumziwa kwamba endapo commissioner ama ofisi husika itapeana ardhi ambayo ilikuwa ya umma kwa mtu binafsi ama shirika, basi ardhi hiyo itatumika kulingana na yale matarajio ama maombi yaliyotolewa. Ni jambo la kuhuzunisha hasa ukiangalia sehemu kama Vipingo Sisal Estate iliyo Kilifi. Hii ilikuwa ardhi ya umma. Wenyeji walikuwa wanaishi pale. Ilipewa wazungu waliotaka kulima mkonge. Hilo lilikuwa ni wazo zuri lakini inavyotendeka saa hizi ni kwamba mkonge haulimwi tena. Wameanza kukata kata ploti na kuuza kwa bei ya juu ilhali ni ardhi ambayo walipewa bure, wenyeji wakifurushwa ili walime mkonge. Hili limetamausha sana watu wa sehemu zile. Linatatiza kwa sababu wakati huu konge halina thamani. Basi mzungu ameona hana haja tena ya kulima. Basi airejeshe ardhi ile siyo kwa Serikali ama county lakini kwa wenyewe. Bado vizazi vipo na kila mtu anajua sehemu yake ilikuwa wapi. Ikiwa ni kuuza, basi wenyeji wauuze. Si kwamba mtu alipatiwa ardhi bure kwa malengo ya kudanganya, kisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}