GET /api/v0.1/hansard/entries/1337424/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1337424,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337424/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Kuna suala lingine ambalo ninafikiri lingeingia katika mswada huu na linahusu wawekezaji ambao hupata ardhi wakafanya mradi kisha baadaye wakimaliza huondoka. Ardhi hii inarudi kwa nani? Kwa mfano, ile kampuni kubwa ya Kwale ambayo inaitwa BaseTitanium, waliweza kuchukua ardhi, wakaelewana na wenyeji, wakachimba, wamemaliza na wameondoka. Kulikuwa taratibu kwamba waweze kurekebisha ardhi ile. Lakini hatimaye, kwa sababu wale ni wazungu wawekezaji na watarudi kwao, ardhi hii itarudi kwa nani? Stakabadhi hii itabaki wapi? Kwa sababu ikibaki hivyo, hata baada ya kuirekebisha utapata ni wale mabwenyenye watakuja na hatimiliki kwamba sasa wao ndio wenyewe."
}