GET /api/v0.1/hansard/entries/1337425/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337425,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337425/?format=api",
"text_counter": 352,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Ningetaka kuangalia kifungu cha 22(2) cha Mswada huu ambacho kinasema kwamba ardhi ya umma isiweze kupeanwa ikiwa kuna mmomonyoko wa ardhi, mafuriko na mambo kama hayo. Hapa ninaona Mhe. King’ara kulingana na utaratibu ama uweledi, mimi kama mhandisi wa masuala haya, isiwe ni kigezo kisichoweza kutolewa. Iwapo yule anayepatiwa, malengo yake… Isiwe kwamba wenyeji hawawezi kuitumia ardhi kwa sababu kuna mafuriko ama mmomonyoko wa ardhi. Lengo ni ardhi kurekebishwa ili iweze kuleta faida kwa wananchi. Basi, hili ni suala ambalo lingetaka kuangaziwa kitofauti badala ya kusema moja kwa moja eti sehemu kama hizo haziwezi kupeanwa."
}