GET /api/v0.1/hansard/entries/1337426/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337426,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337426/?format=api",
"text_counter": 353,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Hali kadhalika, nikiangalia kifungu 22(2)(c) kinazungumzia sehemu ambazo zina maji pia zisiweze kupeanwa. Kwa sababu huu ni wakati wa mtandao wazi, ukiweza kuenda kwa huyu jamaa anayeitwa Google na kuangalia hoteli za kifahari ulimwenguni, utakuta kuna hoteli ambazo zimejengwa chini ya bahari ama kwenye maji. Hizi ni hoteli ambazo wengi wangekuwa na hela za kutosha, wangetamani kulala ndani kabla ya kwenda mbinguni. Kwa hivyo, ukisema moja kwa moja kwamba sehemu kama hizo ziwekewe sheria zisiweze kutolewa, inamaanisha kisheria haitawezekana wawekezaji kuwekeza katika sekta hii ya utalii kwa kujenga mahoteli ya kifahari katikati ya bahari, chini ya maji. Hapo tutakuwa tunawanyima wawekezaji nafasi. Sisi tutajinyima mapato kutoka nchi za kigeni na ajira katika sehemu nyingi - kama sehemu za kwetu - ambazo uchumi zinazotegemea sana ni uchumi wa utalii. Ninaunga mkono Mswada huu. Asante."
}