GET /api/v0.1/hansard/entries/1337428/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337428,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337428/?format=api",
"text_counter": 355,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nimesubiri ya kutosha ili niweze kutia shime mswada huu ambao umeletwa na Mhe. King’ara. Mimi pia ninaungana na wenzangu kuunga mkono kwamba ardhi za umma ziweze kupata stakabadhi. Ni aibu sana kuwa mpaka sasa, miaka 50 tangu tupate uhuru, shule zote za umma hazina hatimiliki. Ziko tu na zinasemekana ni za umma lakini haijulikani stakabadhi zake zipo wapi na ardhi zao ni za aina gani. Nikitilia mkazo maneno yaliyozungumzwa na Mhe. King’ara, imefika wakati hata miradi ya Serikali haina mahali pa kujengwa kwa sababu hakuna ardhi. Hata sisi upande wa National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF) inatubidi mara nyingi tununue ardhi ilhali Serikali ni tajiri kwa ardhi. Ardhi za umma zitolewe stakabadhi. Kisheria, ukiwa na ardhi binafsi ya kiwango fulani lazima itolewe kama public utility . Ikiwa publicutility, ni automatic itakuwa ardhi ya umma. Shida iliyoko ni kwamba lazima tuhakikishe ufisadi katika Wizara ya Ardhi umebanwa ili ufisadi uishe pale. Nina imani utajiri wa ardhi utapatikana. Kwa sababu sisi tuna ardhi ya kutosha, ardhi ya community tayari ni ya umma. Mtu mwenye ardhi ya kibinafsi akijenga estate ya nyumba zaidi ya 30 au 40 za kuuza, pale patakuwa na watoto na ni lazima atawatengenezea mahali pa kucheze. Lazima atatengeneza mahali pa kumwaga taka, mahali pa kuweka zahanati na mahali pa maabadi kwa sababu ya watu watakao kuwa pale kuabudu. Kwa sababu ya ufisadi, hizi sehemu haziko katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}