GET /api/v0.1/hansard/entries/1337429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337429/?format=api",
"text_counter": 356,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "majengo mengi. Haya mambo hayakuanza leo; yalianza wakati wa manispaa kabla ya serikali za ugatuzi. Ugawanyaji wa ardhi hauwezi kupita bila kuonyesha public utility ni zipi. Kwa kuwa mpangaji atapangisha wananchi, hawatatoka juu mbinguni wakianguka chini. ni muhimu wawe na barabara ya kutoka nje na kurudi ndani. Ni muhimu wawe na sehemu maalum ya taka ambayo si ya mpangaji bali mali ya umma. Wale wanaoenda kanisani na muskitini lazima wawe na sehemu ya kuabudu. Wale wanaoabudu Jumamosi pia wawe na sehemu yao ya kuabudu. Ikiwezekana, ardhi za umma zifanyiwe auditing kuanzia wakati manispaa zilipokuweko, ili kama ardhi hizo zingalipo zirudi kwa umiliki wa Serikali. Leo tunapozipatia pesa za NG-CDF – ambazo si nyingi – tunalazimika kuzitumia kununua ardhi. Mheshimiwa King’ara atilie mkazo stakabadhi hatimiliki iwe na nguvu kwa sababu leo unaweza kuwa na hatimiliki na kesho aje mtu aseme hiyo ni karatasi tu uliyobeba. Itakuwa haina maana wewe kuwa na hiyo stakabadhi. Kwa hivyo, ni lazima tutilie mkazo kuwa ikiwa ni hatimiliki, iwe ina nguvu. Ukipewa kutoka kwa Serikali, hakuna mtu atakayekuja akuambie jambo lolote kuihusu. Utapata kuwa mahospitali yetu hayana hatimiliki. Mtu yeyote anaweza kuja akasema ardhi ya hospitali ni yake na wagonjwa wote wakatolewa mbio. Kuhusu suala la uvunjaji, sioni kama ni jambo la busara. Hii ni kwa sababu nchi hii inaongozwa na sheria. Ikiwa mtu anachimba msingi, huwa amepata stakabadhi kutoka serikali ya kaunti. Anachimba msingi na kujenga akiwa na ruhusa zote kisha akishamaliza wewe unakuja kusema ni yako. Hapo ni makosa sana. Hilo siwezi kubaliana nalo. Kwa huu Mswada, ninakubaliana kwamba stakabadhi zitolewe lakini zipewe nguvu. Utakapokuwa nayo, kisheria, hakuna mtu ambaye atakuja kukutingiza. Kwangu Kisauni, kuna matatizo makubwa ya ardhi. Watu wamejenga wakamaliza kisha mtu anakuja anasema atawavunjia nyumba. Hakuna! Wewe ulikuwa wapi wakati ambao walikuwa wakichimba msingi. Ulikuwa wapi wakati walikuwa wanatia jiwe la kwanza? Ulikuwa wapi wakati walikuwa wanatia umeme? Ulikuwa wapi mpaka jengo liwe limeisha ndiposa uje? Utaua watu ambao wamefanya kazi mpaka wamestaafu. Wameweka pesa zao pale na wakachukua rehani na mikopo kutoka benki. Mtawaua Wakenya. Sikubaliani na uvunjaji lakini ninakubaliana na Mswada huu wa ardhi. Mhe. King’ara, umefanya kazi nzuri na nina imani Bunge lote litakuunga mkono. Kwa hayo mengi, asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}