GET /api/v0.1/hansard/entries/1337885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337885,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337885/?format=api",
"text_counter": 379,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": "Unaposafiri katika viwanja vya ndege tofauti ulimwenguni kama kule Amsterdam ama Dubai, unapata kuwa wengi wa maafisa wanaofanya kazi katika viwanja hivyo vya ndege huwa ni Wakenya. Anapokuangalia usoni, yeye hung’amua mara moja kuwa wewe ni Mkenya na anakusalimu na kusema “Habari yako?” ama “Hujambo?” Jambo hilo linaonyesha kuwa tuna rasilimali kubwa sana kama nchi ya watu ambao wamehitimu katika mambo ya uchukuzi wa ndege. Pengine wanaenda kwa nchi geni kwa sababu ya kukosa nafasi za kazi hapa nchini. Tunapozingatia mambo ya uchukuzi katika viwanja vya ndege, nafasi za kazi huwa urubani ama utumishi katika ndege. Lakini ukiangalia upande wa kuzuia ajali au upelelezi wa ajali, maafisa hao hawako kabisa katika nchi yetu ya Kenya. Ninatumai kuwa Mkataba huu hautakuwa karatasi iliyotiwa sahihi bali tutaweka jitihada za kuhakikisha kuwa tumewekeza hela katika uzuiaji na upelelezi wa ajali za anga."
}