GET /api/v0.1/hansard/entries/1337886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1337886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337886/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": "Katika hafla zetu zote za kirasmi hapa nchini, huwa tunaanza kwa kuimba wimbo wa taifa na ule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika ubeti mmoja wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tunasema kuwa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki idumu. Lakini tunapoangalia utendakazi wetu ama jinsi ambavyo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinavyoendeleza biashara zao, tunaweza kuwasiliana katika maswala mangapi? Unapata kuwa tunatafuta nchi zingine za mbali sana kutusaidia katika mikakati yetu na kuendeleza mikataba au mahusiano. Hatujafanikiwa kuhakikisha kuwa tunazingatia kudumu kwa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki. Tunapaswa kuzingatia umoja wa Afrika Mashariki."
}