GET /api/v0.1/hansard/entries/1337889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1337889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1337889/?format=api",
    "text_counter": 383,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Molo, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
    "speaker": null,
    "content": "katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na shida tulizo nazo mipakani mwetu, na sio tu maswala ya ajali za ndege, tungekuwa mbali sana. Ikiwa watu wangeweza kutoka katika nchi moja na kwenda kwa nyingine bila kuulizwa maswali mengi ambayo wanaulizwa kwa sasa katika mipaka yetu, na ikiwa tungeweza kuuza bidhaa zetu bila pingamizi lolote katika nchi za Afrika Mashariki, Jumuiya ya Afrika Mashariki ingeweza kuendelea zaidi, sio tu kama jumuiya, lakini pia kama nchi binafsi. Wakati Wakenya wanaporudi nyumbani baada ya kutembelea nchi zingine, wengi wao husema kwamba wanahuzunika. Wale maafisa ambao wanawapokea wageni, mara nyingi customer service yao, kama tunavyosema kwa kimombo, huwa haifurahishi. Utapata kwamba ni kama wana bidii zaidi kuwatafutia makosa. Wanaangalia begi zao zina simu ngapi ama wamebeba vitu ngapi vya hela fulani ili waweze kuwaitisha ushuru ingawa ni sheria ambayo tumepitisha kwamba huwezi kuleta nchini kitu chochote ambacho kimepitisha US$500. Lazima walipe ile ushuru. Mara mingi unapata vile tunavyowaeleza hawa Wakenya na wageni wengine wanapokuja katika nchi yetu ya Kenya inafanya wasitamani kurudi katika nchi yetu. Hata tunapounga mkono huu Mkataba, tunawaomba wale wafanya kazi ambao ni sura yetu ya nchi ya Kenya, wakati mgeni anapokuja ama vijana wetu walioenda kazi ng’ambo wakirudi nyumbani, wawe waangalifu sana jinsi wanavyowaongelesha hao wageni kwa sababu hiyo inawafanya wajue kama watakuja katika nchi yetu tena. Tunaomba tuwaongeleshe wageni wetu na watoto wetu ambao wanarejea nyumbani kutoka kazi kwa njia ya heshima na tuwakaribishe kwa vishindo na nderemo ili wajisikie kwamba wako nyumbani ili hata wanapotafuta riziki katika nchi zingine, wahisi kwamba wamekosa kuja nyumbani na wakikuja nyumbani wapate wanapokelewa na furaha. Kwa hayo machache, Mhe. Spika wa Muda, ninaunga mkono Mkataba. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}