GET /api/v0.1/hansard/entries/1338058/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1338058,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338058/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii na mimi niweze kumuunga mkono dada yangu, Mhe. Donya, upande wa mgao wa El Nino. Ni dhahiri kuwa tunaelekea kwenye msimu wa mvua, msimu ambao saa hizi familia nyingi hawana amani wala furaha. Nikizungumza kuhusu eneo gatuzi langu la Mombasa, watu wengi huathirika sana na mafuriko ya El Nino . Kwa hivyo, ningeomba Serikali… Miaka nenda miaka rudi, Mombasa hatujawahi kupata sisi mgao wa kuweza kukabiliana na madhara ya El Nino . Watu wamehangaika. Wanapata mafuriko na nyumba zao zinabomoka mpaka inabidi kama Mama Kaunti niingie mfukoni kuangalia mapeni kuwasaidia. Mhe. Spika, inatamausha wakati kuna bajeti ambayo imepitishwa ya kuweza kuwasaidia hawa watu. Ninaomba Serikali iangalie kwa usawa kaunti zote, ikiwemo kaunti ya Mombasa."
}