GET /api/v0.1/hansard/entries/1338216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338216,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338216/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Maradhi yamekuwa donda sugu katika jamii yetu. Yamekuwa yakisambaa kwa haraka. Watu wakienda katika hospitali kubwa wakiwa na maradhi ya kusambaa haraka, wanaweza kusambaza sehemu kubwa sana katika taifa. Mswada huu wa leo utawezesha community healthpromoters wasaidie watu katika majumba yao, ama wapate msaada katika zile hospitali ndogo ambazo ziko karibu nao. Ndiyo maana ninasema kuwa huduma ikizidi kwenda mashinani, basi inapatia Serikali wepesi wa kuweza kumudu na kutenda kazi kwa ubora. Ni dhahiri shahiri kuwa hata watoto wetu ambao wamesomea udaktari watapata nafasi kule mashinani. Hizi hospitali ndogo zitawezeshwa kukusanya mapeni yao ya kuendeleza shughuli, ili wasiweze kuanguka katika mitihani ya kukosa namna ya kuendeleza hospitali. Kwa hivyo, wana haki na usawa wa kuajiri madaktari ama nurses wao kule chini, ili wapatie wananchi huduma kwa wepesi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}