GET /api/v0.1/hansard/entries/1338231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338231,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338231/?format=api",
    "text_counter": 308,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe Spika wa Muda. Mswada huu ni muhimu sana kwa sababu utatusaidia kushughulikia changamoto nyingi zilizoko upande wa afya. Tuna changamoto nyingi. Kwa mfano, michango kwa ajili ya bili za hosipitali na kupunguza watu kusafiri kwenda nchi jirani kama Tanzania na India kwa ajili ya kutafuta matibabu. Huwa tunafanya michango kwa watu ili waweze kusafiri nchi hizo. Matibabu ya nchi hizo siyo eti ni bora kuliko Kenya. Kenya ina madaktari wazuri na hosipitali nzuri. Shida ni kwamba gharama ya matibabu iko juu. Mswada huu utatusaidia kuondoa hisia wakati watu wanapotaka kuzika maiti ya watu wao lakini hawawezi kwa sababu ya mwili kuzuiliwa katika hosipitali kwa sababu ya bili. Hospitali nyingi, ziwe za serikali au za kibinafsi, huzuia maiti. Kuna sheria inayosema kwamba mwili usizuiliwe hospitalini, lakini mpaka sasa miili hushikwa na huwa ngumu, hasa kwetu sisi waislamu ambapo tunataka kuzika kwa haraka. Hatuwezi kutoa maiti kwa sababu ya bili za hosipitali. Mswada huu utatusaidia kuhakikisha kuwa wanyonge pia wamepata huduma. Kwa mfano, watu wa Basuba, kwa sababu ni wachache, huwa hawapati huduma saa zingine kwa sababu kura zao ni kidogo. Magavana wanaangalia pale ambapo kuna kura nyingi ndipo wapeleke huduma pale. Huu Mswada utahakikisha kuwa hakuna kuangalia jamii ina kura ngapi. Kila mtu atapata huduma. Inasikitisha kuwa mpaka sasa kuna sehemu nyingine, hata baada ya ugatuzi, ambapo wadi nzima haina hospitali. Matatizo yakitokea kule kwetu Basuba Wadi, tunabebwa na Majeshi ya Ulinzi kupelekwa hosipitali ya rufaa ya King Fahd. Mswada huu utaondoa matatizo kama hayo. Mswada huu pia umezungumzia kuhusu wanyonge na maskini— the indigent . Ni vyema Mswada huu ukipita, tuhakikishiwe kwamba wanyonge na maskini watakaosaidiwa wamechaguliwa katika kila eneo Bunge ili tuwajue kwa majina ndiposa wengine wasisahauliwe. Mswada huu ni mzuri kwa hivyo ni vyema utusaidie. Mswada huu utasaidia pesa zifike kule mashinani kwa watu ambao hawatambuliki na wametengwa. Pia, utasaidia pale ambapo kuna changamoto za usafiri, kama eneo Bunge langu kule Lamu Mashariki. Nimefurahishwa sana na Mswada huu. Ninapongeza Seneti na Kiongozi wa Chama Cha Walio Wengi. Ni muhimu Mswada huu upite kwa haraka ili watu wapate kusaidika. Yafaa tuupitishe hata kama ni hivi leo. Asante, Mhe. Spika wa Muda."
}