GET /api/v0.1/hansard/entries/1338367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338367,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338367/?format=api",
    "text_counter": 444,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Bwana Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ya kuchangia Mswada huu wa afya ambao umeletwa Bungeni na Kamati husika. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu katika mambo ya ufundishaji wa afya, tutakuwa na wale maafisa ambao wamefunzwa pale nyumbani na watakuwa wakitembea vijijini kuhakikisha kuwa watu wako na afya njema kwa kuwapima. Hilo ndilo limenifanya niunge Mswada huu mkono. Mswada huu unafanana na ule ambao umetoka Seneti unaosema kuwa pesa inayokusanywa na kila hospitali pale nyumbani itatumika kwa minajili ya wagonjwa katika eneo hilo. Mswada huu utaleta usaidizi kubwa. Hakuna kitu kizuri kama wananchi wa Kenya kujipima kabla ya kuwa wagonjwa. Unapopimwa kabla ya kuwa mgonjwa, inakuwa rahisi sana afya yako kutekelezwa na hospitali husika. Vilevile, ninaunga Mswada huu mkono kwa sababu maafisa ambao watapatiwa nafasi kuelimisha wananchi kule nyumbani watakuwa wakitoka kwa kila kijiji. Kwa hivyo, ninaunga mkono, nimefurahi sana na ninajua wananchi wa Nakuru watafurahia na watafaidika kwa huu Mswada. Kwa hayo machache, Mhe, Spika wa Muda, ninaomba kuunga mkono. Asante sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}