GET /api/v0.1/hansard/entries/1338488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338488,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338488/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu wa Spika, kwa kunipa nafasi nami nichangie. Kati ya sehemu zilizoathirika na mambo ya mihadarati, Lamu ni zaidi. Utasikitika ukifika Lamu uone jinsi vijana wameathirika. Mihadarati pia inachangia utovu wa usalama na inaathiri uchumi wa Lamu. Wale vijana wanaotumia mihadarati wanahitajika wawe na Ksh1,400 kwa siku. Kama hawana kazi, inawabidi waibe ndiposa wapate dawa hizo. Wanaenda kuibia wenye mashamba haswa wakulima wa minazi ambao mwishowe hawapati kuvuna. Wafugaji mbuzi na kuku pia wanaibiwa. Athari ni kwa wale wanaotumia mihadarati na pia wale ambao hawatumii. Wale wanaotumia mihadarati hawawezi hata kuoa na inakuwa shida kubwa. Vituo vya ukarabati vikiwekwa vitasaidia sana. Lamu Magharibi ina vituo viwili vya ukarabati vikiwa Red Cross na kituo cha watu binafsi. Lamu Mashariki haina kituo hata kimoja. Itakuwa vyema kuzingatia watu wetu ambao hawana huduma hizo. Watu wetu wa Lamu Mashariki wanakaa kwenye visiwa vya bahari na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}