GET /api/v0.1/hansard/entries/1338489/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338489,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338489/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "wanapata changamoto kumpeleka mtu Lamu ijapokuwa ni karibu. Ninampongeza Mjumbe aliyeleta Hoja hii kwa jambo hili la maana sana. Wanaotumia mihadarati wanaweza kutumika vibaya kama hatuwabadilishi. Tunaishi kwenye boundary ya Somalia. Ni rahisi mtu anayetumia mihadarati kutumika vibaya na wanakua vulnerable . Wanaweza tumika vibaya mpaka tushangae. Saa zingine pia unaona kama hili jambo haliangaliwi. Wananchi kule wanafikiria kuwa wanaletewa mihadarati, na kila anayeuza mihadarati anajulikana, lakini hakuna hatua inachukuliwa. Sisi tunaletewa mihadarati ilhali wengine wanasaidiwa. Imekuwa labda ni kama ni kusudi Serikali inafanya. Lakini, alhamdulillah, ninamshukuru mwenyezi Mungu kuwa kuna mikakati hii Serikali inachukua. Ninawapongeza. Hakika hii ikipelekwa kwa Waziri Kindiki ataishughulikia vilivyo. Hata kama ni kwa mfuko wa hiyo Ministry yake, ataifanya. Maanake amefanya mambo mazuri Lamu, na tunaipongeza Serikali. Kwa hili tunaomba watufanyie zaidi na zaidi ili watoto wetu watoke katika hizo mbinu. Pia, kabla hizi rehabilitation centres kutengenezwa kama kila Level 4 hospital itawekwa ile"
}