GET /api/v0.1/hansard/entries/1338499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338499,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338499/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili kuchangia katika mdahalo huu wa mambo ya mihadarati. Ni jambo la kusikitisha na kutamausha, haswa vijana wengi kutoka Pwani wamepoteza maisha na mwelekeo kwa sababu ya utumiaji wa mihadarati. Mihadarati sasa ni tisho kwa usalama wa vijana wetu hasa wale ambao wako shule. Mambo ya mihadarati yamezungumziwa kwa muda mrefu, lakini kila uchao tunaendelea kuzungumzia matumizi ya mihadarati. Shirika la National Authority for the Campaign Against Alcohol and Drug Abuse (NACADA) ambalo linatakikana kuhakikisha kwamba mambo ya mihadarati haifanyiki linafanya nini? Na kila mwaka linapatiwa bajeti na Bunge hili ili liweze kutatua shida hii. Hatuwezi kuendelea kuwalaumu wale wanaotumia mihadarati. Tunataka tujue kupitia shirika la ujasusi National Intelligence Service (NIS) ni kina nani wanaleta mihadarati katika nchi hii. Tukitaka kusitisha utumizi wa mihadarati na watoto wetu na vijana wetu, haswa kwa mashule, ni lazima tuangalie shida ni gani. Na ikiwa Serikali inawajua wale ambao wanaleta mihadarati, kwa nini hakuna hatua ambazo zimechukuliwa kwa muda huu wote? Tuseme Serikali inachangia kwa sababu kama mtu anauza mihadarati na anajulikana, kwa nini hawezi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}