GET /api/v0.1/hansard/entries/1338500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1338500,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338500/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": "kuchukuliwa hatua? Mimi nimeunga mkono kwamba tuweze kupanua zahanati ambazo zinarekebisha hawa vijana wetu ambao wanaendelea kutumia mihadarati. Lakini ni ghali mno, na katika kusitisha hii lazima Serikali ijitokeze. Na lile shirika la NACADA ambalo limepatiwa jukumu liweze kujikakamua ili tuweze kusitisha utumiaji wa mihadarati kati ya vijana wetu. Vijana wataendelea kutumia mihadarati kwa sababu hawana njia ya mapato. Sasa kujiliwaza wanaona ni njia moja ya kutumia mihadarati ili wapoteze mawazo. Mihadarati imeharibu familia nyingi. Vijana wanaotumia mihadarati hawawezi hata kuoa kwa sababu wakipata chochote kidogo wanakimbilia mihadarati. Wanachukua hata vyombo vya nyumbani wanaenda kuuza ili waendelee kula mihadarati. Ikiwa tunataka kama taifa kusitisha, kusimamisha, na kukomesha kabisa mambo ya mihadarati, ni lazima tuungane kama taifa tupigane na janga hili la mihadarati. Tuweze kuleta viongozi wote wa kidini na wa kijamii, na taasisi zote ili kwa taifa tuseme mambo ya mihadarati hatutaki tena katika nchi yetu. Na ni lazima Serikali ichukue hatua kali kwa wale ambao wanaleta mihadarati na wanajulikana, ila Serikali inanyamaza. Ni lazima kama taifa tujitokeze kimasomaso na kusema kwamba lazima tulinde maisha ya vijana wetu hasa wale ambao wako shuleni. Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii."
}