GET /api/v0.1/hansard/entries/1338510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1338510,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338510/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaunti ya Mombasa, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii nizungumze kama Mama Kaunti wa Mombasa. Ninalia sana kwa sababu tunahitaji hizi sehemu za marekebisho ama rehabilitation centres . Kila mtu anajua kuwa Mombasa imeathirika zaidi na dawa za kulevya. Watoto wetu wamekuwa zombies, wanashika panga, hawaoi, wakisimama mahali pamoja wanaenda mpaka chini na kurudi juu kwa sababu ya dawa za kulevya. Mkiona wanavyofanya, mtashangaa sana. Wakati mwingine, wengine wanaanza kutembea mwendo wa pole pole na kuzungumza kwa kuvuta maneno yao sana."
}