GET /api/v0.1/hansard/entries/1338512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338512,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338512/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaunti ya Mombasa, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Kama Mama Kaunti, nimekuwa nikiwaregesha watoto shuleni. Wengi wao ni watoto wa kike waliokua wameathirika na dawa za kulevya. Wakishavuta zile dawa, walikuwa wanajiingiza katika mambo machafu, ukahaba, na mambo mazito sana, ilhali ni watoto wadogo wa miaka 14, 15 au16. Jambo hilo lilikuwa linanitamausha sana. Wengi wamenishukuru na kusema kuwa walikuwa wameingia katika mambo mazito sana. Siwezi kurekebisha mambo hayo peke yangu. Lazima nipate usaidizi kutoka kwa Serikali ili tuhakikishe kuwa tutapata"
}